AZZURI YAWAKALISHA 2-1 SIMBA WATATU KOMBE LA DUNIA, BALOTELLI KIBOKO...
Mario Balotell akiifungia bao la pili Italia
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/azzuri-yawakalisha-2-1-simba-watatu.html
TIMU ya Taifa ya England `Simba
watatu` imeanza vibaya kombe la dunia baada ya kukubali kichapo cha
mabao 2-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Italia maarufu kwa jina la Azzuri
mjini Manaus katika mchezo wa kundi D.
Italia walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 35 kupitia kwa Claudio
Marchisio, lakini katika dakika ya 37, Daniel Sturridge aliisawazishia
England bao hilo akiunganisha krosi nzuri iliyochongwa na Wayne Rooney
kutoka wingi ya kushoto.
Daniel Sturridge akiisawazishia England bao la kwanza
`Supa` Mario Balotelli ndiye aliwaua England baada ya kuandika bao la pili kwa njia ya kichwa katika dakika ya 50.Kikosi
cha England kilichoanza: Hart, Johnson, Cahill, Jaglielka, Baines,
Gerrard, Henderson, Sterling, Rooney, Welbeck and Sturridge
Kikosi cha Italia kilichoanza:
Sirigu, Chiellini, Paletta, Barzagli, Darmian, De Rossi, Pirlo, Veratti,
Candreva, Marchisio and Balotelli.
Claudio Marchisio akitandika shuti kali na kuifungia Azzurri bao la kuongoza.