Flatnews

Iraq yaomba msaada wa kijeshi kwa Marekani


Ndege ya Marekani isiyotumia rubani-Drone
Ndege ya Marekani isiyotumia rubani-Drone

Mkuu wa majeshi ya Marekani anasema Iraq imeiomba Marekani kusaidia kufanya mashambulizi ya anga ili kupambana na wanamgambo wa ki-Islam wa ki- sunni ambao wamechukua udhibiti wa miji muhimu ya kaskazini na wanaitishia kuishambulia Baghdad.

Mwenyekiti wa baraza la wakuu wa majeshi, Jenerali Martin Dempesy, ali-iambia kamati ndogo ya baraza la seneti la Marekani hapo jumatano kwamba serikali ya Iraq imeshindwa kuwalinda wananchi wake na amesikitishwa sana na jambo hilo.

Naye waziri wa ulinzi wa Marekani, Chuck Hagel alisema viongozi wa kishia nchini Iraq, hawajawahi kutekeleza jukumu lao la  kuunda serikali ya umoja wa kitaifa pamoja na wasunni na wakurdi.

Wakati huo huo, akisafiri kuelekea Colombia, Makamu Rais wa Marekani, Joe Biden alizungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Iraq, Nouri al-Maliki pamoja na viongozi wa kisuni na wa kikurdi. Alisisitiza juu ya umuhimu wa serikali ya umoja nchini Iraq  ambayo itaweza kukabiliana na kitisho kinachosababishwa na  wanamgambo, kwa wa-Iraq wote

Post a Comment

emo-but-icon

item