Flatnews

WAZIRI LAZARO NYALANDU AONGOZA MATEMBEZI YA KUPIGA VITA UJANGILI WA TEMBO.


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (MB) akipokewa na Bi. Raabia Hawa, Mratibu wa matembezi ya kupiga vita ujangili wa tembo yaliyoanzia Hifadhi ya Taifa Arusha na yanatarajiwa kumalizikia Nairobi, Kenya tarehe 28 mwezi huu.
Matembezi yakaanza katika nyika eneo la Sanya Juu
Wageni hawa nao kutoka Australia walishiriki matembezi hayo
Mwendo ulipokolea na makoto yalivuliwa ili kuwa na wepesi zaidi.

Watembeaji wakipumzika kidogo kabla ya kuendelea na matembezi.

Kundi kubwa la nyuki liliwafanya watembeaji kuinama kwa muda kupisha nyuki wapite.

Bi. Raabia Hawa akifuta machozi baada ya kuguswa na hotuba ya Waziri Nyalandu kuhusu askari aliyepoteza maisha yake katika Pori la Akiba la Maswa kwa kuuwawa na Majangili.

Watembeaji katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu. 
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

Post a Comment

emo-but-icon

item