ICC yasema ina ushahidi dhidi ya Gbagbo
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/icc-yasema-ina-ushahidi-dhidi-ya-gbagbo_13.html
Mahakama ya kimataifa ya jinai
ICC imesema kuwa ina ushahidi wa kutosha kumfungulia mashitaka ya
uhalifu wa kivita rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo.
Anatuhumiwa kwa mauaji, ubakaji, jaribio la mauaji na udhalimuBwana Gbagbo mwenye umri wa miaka 69 ambaye ndiye Rais mstaafu wa kwanza kushitakiwa katika mahakama ya ICC anasisitiza kuwa hana hatia yoyote.
Anasema kuwa yeye ni mwathiriwa wa njama ya wakoloni wa zamani wa Ufaransa kumtoa uongozini
Majaji watakaoendesha kesi hiyo waliamua kuwa upande wa mashitaka haukuwa na ushahidi wa kutosha kumshutumu bwana Gbagbo lakini tarehe bado haijapangwa
Alikuwa rais wa Ivory Coast kuanzia mwaka 2000 hadi mwezi wa Aprili 2011 alipokamatwa na wanajeshi watiifu kwa rais Alassane Ouattara aliyeungwa mkono na askari wa kifaransa
Bwana Gbagbo ndiye rais mstaafu wa kwanza kukamatwa na kuwekwa kizuizini na mahakama ya ICC ingawa Slobodan Milosevic kutoka Yugoslavia na Charles Taylor kutoka Liberia walihukumiwa katika maalum Hague
