HATIMAYE BINGWA WA MBIO ZA MAGARI, MICHAEL SCHUMACHER APATA FAHAMU BAADA YA MIEZI 6, NI BAADA YA AJALI MBAYA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/hatimaye-bingwa-wa-mbio-za-magari.html
Mwanaspoti anayefahamika katika mashindano ya uendeshaji wa magari ya langalanga au F1 Michael Schumacher amepata fahamu.
Michael Schumacher alitoka hospitalini Grenoble na ataendelea kuishi kwa hali yake ya kawaida,familia yake ilisema.
Schumacher
alilazimika kudungwa sindano ya kupoteza fahamu baada ya kupata
majeraha mabaya kichwani huko French Alps tarehe 29 Disemba.
Madaktari walichukua hatua hiyo ili kusaidia ubongo uliovimba wa mshindi huyo wa mara saba kunywea.
Familia
yake iliendelea kwa kushukuru wote waliomtumia jumbe za kumtakia afueni
ya haraka kwa kusema zilimtia moyo,pia waliwashukuru madaktari
waliomhudumia alikolazwa katika hospitali ya Grenoble,kusini -mashariki
mwa ufaransa.
Schumacher alistaafu kutoka kwa mashindano ya Langalanga mwaka 2012
Sabine Kehm ambaye ndiye meneja wake alisema katika taaarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia yake.
Hapo awali familia yake ilikuwa imeonya kuwa toka mwanzoni itakuwa hali ngumu sana kwa Michael.
Wapelelezi
katika ajali hiyo wanasema Schumacher alikuwa kwa mwendo wa kasi kama
mwenye uzoefu wa mchezo huo wakati wa ajali hiyo Meribel
Alikuwa akiteleza kwenye theluji alipoanguka na kugonga mwamba.
Schumacher alistaafu kutoka mchezo wa F1 mwaka wa 2012 baada ya kuwa kwa safu hiyo kwa miaka 19.



