Flatnews

BIBLIA YATUMIKA KUTAKA KUHALALISHA BANGI

Jani la mmea wa bangi. ©Greens Man Page


Jani la mmea wa bangi. ©Greens Man Page
Wakati siku ya Jumapili ikikutanisha watu wengi kwenye nyumba za ibada, hali imekuwa tofauti kwa seneta Constance Johnson wa jimbo la Oklahoma huko Marekani, pale ambapo amenukuu kifungu cha Biblia kutoka kitabu cha Mwanzo 1:29, akisema kwamba Mungu aliweka kila kitu kitumike na binadamu, hivyo ataendesha kampeni nchini humo ili mmea wa bangi uhalalishwe rasmi kwa matumizi ya binadamu.
"Mungu ameumba jani hili la kipekee na la maajabu, na sote tunajua kwamba limekuwa likidharauliwa kwa kipindi cha miaka 100 iliyopita" Seneta huyo kutoka kambi ya Democrats ananukuliwa akisema, "Ni muda muafaka sasa wa kubadili hali hiyo hapa Oklahoma" anamalizaia kusema seneta huyo akiwa sanjari na wakili David Slane.
Kitabu cha Mwanzo 1:29 kinaeleza; "Mungu akasema, Tazama nimewapa kila mche utoao mbegu ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;" Na hapa ndipo msingi wa Seneta huyo kuanza kukusanya sahihi za watu jimboni humo ili waweze kufikia 160,000 ndani y miezi mitatu kutoka kwa watu waliosajiliwa kupiga kura ilikuanza kupata uhalali.
Tunajua kuna watu wana chuki nasi, na wengine hata wanatumabia twende motoni (go to hell), lakini sisi hatujali, tunataka sauti ya watu isikike licha ya vikwazo vingi ama licha ya watunga sera wanavyoona mambo, anamalizia kueleza Seneta huyo kwa wananchi.
Muswada ambao seneta huyo atakuwa anasainisha watu unataka kwamba, gramu 28 za bangi zitumike kwa matumizi binafsi (starehe), huku gram 85 ziidhinishwe kutumika kwenye mahospitali.

Post a Comment

emo-but-icon

item