Baada ya mashambulizi mawili Kenya, Hii ndio kauli ya Rais Kenyatta.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/baada-ya-mashambulizi-mawili-kenya-hii.html
Rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta amesema kuwa mauaji yaliyofanywa katika mji wa
Mpeketoni, Pwani ya Kenya hayakufanywa na kundi la wapiganaji wa
kiislamu la Al Shabaab.Kauli ya Rais Kenyatta inakuja siku moja baada ya
kundi hilo kukiri kufanya mauaji yaliyotokea Mpeketoni Jumapili
usiku.Akitoa hotuba yake ya kitaifa, Rais Kenyatta pia amesema maafisa
wa polisi Mpeketoni ambao walifanya uzembe hadi kutokea mashambulizi
hayo watashtakiwa.
Al Shabaab lilikiri katika taarifa kwa vyombo vya habari kuwa ndilo lilifanya mauaji hayo Jumatatu jioni.
Mauaji
zaidi yalifanyika usiku wa kuamkia leo licha ya taarifa ya Al Shabaab
kusema kuwa washambuliaji walioshambulia Mpeketoni walikuwa wamerejea
salama nchini Somalia.
Uharibifu
mkubwa ulishuhudiwa katika mji huo huku washambuliaji wakichoma hoteli
na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari waliyoyatumia kwa
usafiri wao.
Kenyatta amesema kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanaochochea uhasama miongoni mwa jamii.