Unadhani wewe ni shakibi wa soka?
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/unadhani-wewe-ni-shakibi-wa-soka.html
Kutana na Mbwa anayependa soka kuliko mashabiki wa soka wenyewe.
Mbwa huyu nchini Marekani wakati wote anakuwa mbele ya televisheni wakati michuano ya kombe la dunia inapokuwa inaendeleaNdio wengi wanamuita rafiki mkubwa na wa karibu sana kwa binadamu.
Mbwa huyu anajulikana kama Georges, ambaye uraibu wake ni soka na ambaye anapenda sana kukaa mbele ya televisheni kwa masaa mengi akitazama kombe la dunia.
Bila shaka Georges anapenda sana soka , lakini swali ni je anaunga mkono timu gani au yeye bora aone tu watu wakicheza kwenye televisheni na kukimbilia mpira huku na kule.
Unadhani wewe ni shabiki wa soka, basi humshindi Mbwa huyu ambaye hachoki kutazama kombe la dunia.
Hata hivyo, mmiliki wa Mbwa huyu anasema kwa Georges,haijalishi nani anayecheza , kushinda au kushindwa.
Lakini ana haki ya kufurahia mchezo huu kama mtu yeyoye ule.
George akitizama mechi kati ya Argentina na Bosnia ambayo ilishuhudia bao la Lionel Messi lililoipa ushindi timu hiyo.