Angalia Picha Ngamia mtabiri wa mechi za kombe la dunia na matokeo ya utabiri wake
http://samchardtz.blogspot.com/2014/06/angalia-picha-ngamia-mtabiri-wa-mechi.html
Kwenye
miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na matumizi ya wanyama na viumbe
wengine kwenye kutabiri matokeo ya mechi za soka hasa kwenye michuano
mikubwa kama kombe la dunia.Mwaka 2010 wakati wa WOZA, nchini Ujerumani
kulikuwa na Pweza ‘Octopus Paul’ ambaye alitabiri mechi zote na akapatia
kila utabiri, mwaka huu amekuja Ngamia aitwaye Shakeeen kutoka Dubai
ambaye nae alianza kutabiri tangu siku ya kwanza.Shakeen ambaye
anamilikiwa na shabiki mmoja wa timu ya soka ya Al Wasry ya Dubai,
alitabiri mechi zote za ufunguzi na akapatia, akatabiri ushindi wa Italy
dhidi ya England akapatia, jana akaitabidi ushindi Ufaransa na
Argentina akapatia tena.
Pia ameitabiria Ureno kushinda mechi ya leo dhidi ya Ujerumani.

