WAWILI WAFA KATIKA AJALI YA PRADO MBEYA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/wawili-wafa-katika-ajali-ya-prado-mbeya.html
Watu
wawili Rehema Mwamaso [30], mkazi wa Sumbawanga na mwanaume mmoja
ambaye bado hajafahamika jina wala makazi yake,umri kati ya miaka 30-40,
walifariki dunia papo hapo kufuatia ajali iliyotokea wakiwa katika gari
T.620 CTL aina ya Toyota Land Cruiser Prado lililokuwa likiendeshwa na
dereva Robert Jubery Mwaihoje [61],mkazi wa Sumbawanga.Tukio
hilo limetokea tarehe jana majira ya saa 2:00 asubuhi huko katika
kijiji na kata ya Nakawale,tarafa ya Ndalambo,wilaya ya Momba, mkoa wa
Mbeya, barabara ya Sumbawanga/Tunduma. Katika tukio hilo watu wengine
watatu walijeruhiwa akiwemo dereva wa gari hilo na wanawake wawili ambao
bado hawajafahamika majina na makazi yao. Chanzo cha ajali hiyo ni
mwendo kasi, taratibu zinafanywa ili dereva afikishwe mahakamani.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed
Msangi anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapoyumia vyombo vya
usafiri kwa kuzingatia sheria na alama za barabarani ili kuepuka ajali
zinazoweza kuepukika. Aidha anatoa rai kwa wananchi kufika katika kituo
cha afya tunduma kwa ajili ya utambuzi wa marehemu na majeruhi.
