WASANII MRUDIENI MUNGU!
KUFUATIA kifo cha msanii mkongwe wa filamu Bongo, Adam Kuambiana, msanii mwenzake, Salma Salmin ‘Sandra’ amewataka wasanii kubadili...
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/wasanii-mrudieni-mungu.html
KUFUATIA kifo cha msanii mkongwe wa filamu Bongo, Adam Kuambiana, msanii mwenzake, Salma Salmin ‘Sandra’ amewataka wasanii kubadili mfumo wa maisha na kumrudia Mungu.
Akizungumza
katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar ulipokuwa mwili wa
Kuambiana kabla haujahamishiwa Muhimbili, Sandra alisema ameumizwa sana na
kifo cha msanii huyo kwani kimekuwa cha ghafla sana hivyo ni fundisho
kwao wasanii kwamba wanatakiwa kumrudia Mungu na kuwa watu wa sala muda
wote kwani kifo kipo na hakina muda maalum.
Aliongeza
kuwa haifai wasanii kuwa na mabifu ya kijinga badala yake wapendane
kwani hawajui kifo kitawakuta wakiwa wanafanya nini.
