OSCAR PISTORIUS KUFANYIWA UCHUNGUZI WA KIAKILI KWA MWEZI MMOJA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/oscar-pistorius-kufanyiwa-uchunguzi-wa.html
JAJI
katika kesi inayomkabili Oscar Pistorius wa Afrika Kusini anasema kuwa
mwanariadha huyo lazima aanze kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kuanzia
Jumatatu wiki ijayo kwa muda wa mwezi mmoja kubaini hali yake kiakili
alipomuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Jaji
Thokozile Masipa aliamuamuru Pistorius kua awe anakwenda katika
hospitali ya maradhi ya kiakili ya Weskoppies mjini Pretoria kila siku
kuanzia tarehe 26 mwezi Mei.
Amri ya
jaji inakuja baada ya shahidi mmoja wa upande wa mashitaka kusema kuwa
mwanariadha huyo anakumbwa na matatizo ya kuzongwa na mawazo pamoja na
kuwa na wasiwasi wakati wote.
