NDEGE YA UINGEREZA YAHARIBIKIA NIGERIA
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/ndege-ya-uingereza-yaharibikia-nigeria.html
Ndege ya Uingereza iliyoharibikia kazini na kulazimika kutua Senegal ili kutengezwa
Ndege ya
kijasusi ya Uingereza iliyokuwa katika harakati za kutafuta zaidi ya
wasichana miambili waliotekwa nyara nchini Nigeria, imelazimika kutua
nchini Senegal kutokana na hitilafu.
Ndege
hiyo iliondoka Uingereza Jumapili kujiunga na juhudi za kimataifa za
kuwatafuta wasichana waliotekwa nyara na Boko Haram na sasa imetua
nchini Senegal kutengezwa.
Waziri wa
ulinzi wa Uingereza mjini London amesema kuwa ndege hiyo ambayo
iliondoka Uingereza Jumapili kusaidia wanajeshi wa Nigeria kuwasaka
wasichana waliotekwa nyara, nchini Nigeria zaidi ya mwezi mmoja
uliopita.
Wasichana hao walitekwa nyara zaidi ya wiki tano zilizopita na kundi la wapiganaji waisilamu la Boko Haram.
Nchi
kadhaa zikiwemo Uingereza, Marekani na Israel zinasaidia jeshi la
Nigeria kwa ujasusi katika harakati za kuwasaka wasichana hao ambao Boko
Haram inataka serikali ya Nigeria ibadilishane na wafungwa wa kundi
hilo.
Jeshi la
Marekani linatumia ndege zenye rubani na zile zisizo na rubani kusaidia
juhudi za Nigeria kuwatafuta wasichana hao.Chanzo BBC Swahili
