Flatnews

MZOZO WA THAILAND WAONGEZEKA


62FA11BB-02EF-4970-AFC0-84F558DC1B33 w640 r1 s 792b7

Na Hudgu Ng'amilo
Thailand inasema imeimarisha ulinzi kabla ya maandamano ya leo Jumatatu kati ya makundi yanayounga mkono serikali na yale yanayoipinga.
Hatua hiyo inafuatia kujeruhiwa kwa watu wawili karibu na makao makuu ya serikali Jumamosi jioni katika mlipuko wa gruneti.
Katika tangazo kupitia televisheni ya kitaifa, maafisa wa serikali ya muda walionya watu wakae mbali na maeneo ya maandamano hayo kwa usalama wao.
Waandamanaji wanaopinga serikali hiyo wametoa mwito kuteuliwe Waziri Mkuu anayekubalika na pande zote kesho.
Afisa wa ngazi ya juu wa ulinzi Tharit Pengdit anasema jaribio la kumteuwa Waziri Mkuu ambaye hakuchaguliwa huenda likatumbukiza Thailand katika ghasia zaidi na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe.
CHANZO SAUTI YA AMERICA

Post a Comment

emo-but-icon

item