Flatnews

Mwanariadha wa kike achumbia msichana



Mwanariadha maarufu wa kike nchini Afrika Kusini, Caster Semenya
Mwanariadha maarufu wa kike nchini Afrika Kusini, Caster Semenya haishi kuandamwa na visa, wakati huu akidaiwa kwamba amejipatia mchumba wa kike.
Hii si mara ya kwanza kwa Semenya kukumbwa na visa, safari hii amekumbwa na kashfa akiwa katika maandalizi ya kuelekea katika mashindano makubwa ya Jumuiya ya Madola mwezi huu Scotland.
Mwanariadha huyo amewahi mara kadhaa kunyakua medali ya dhahabu kwenye mashindano ya kimataifa ya mbio za mita 800 na mita 1500.
Mwaka 2008 aliibuliwa tuhuma kwamba anatumia dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku michezoni, baada ya hujuma hiyo kushindikana, likaingia suala la kumpima jinsi kwa madai kwamba anaonekana kuwa na jinsi ya kiume kwa kuwa uwezo wake katika mashindano sawa na wanaume.
Pamoja na mvutano huo, akashinda medali ya dhahabu na kuendelea na taratibu nyingine za upimaji huo, suala lililozua mvutano mkubwa kati ya Afrika Kusini na Shirikisho la Michezo ya Riadha la Kimataifa (IAAF).
Mapya yaibuka
Mwaka huu, wakati akiwa katika maandalizi ya kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola, mapya yameibuka.(Martha Magessa)
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vingi vya habari vya Afrika Kusini, mwanariadha huyo anadaiwa kutoa mahari kwa familia ya mwanadada anayedaiwa kuwa mchumba wake, Violet Raseboya.
Imeelezwa kwamba mahari hiyo ya Rand 25,000 sawa na Sh4 milioni za Tanzani,) imepelekwa kwa familia ya mchumba huyo iliyoko Polokwane Jimbo la Limpopo na ikapokewa na wazazi wa Violet.
Uhusiano usio wa kawaida
Vyombo vya habari nchini Afrika Kusini tayari vimeripoti kuwa Semenya (23) amekuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda sasa na mwanariadha mwenzie wa kike, Violet.
Mwanariadha huyo aligonga vichwa vya habari kote duniani mwaka 2009 alipompiku Janeth Jepkosgey wa Kenya na kutwaa ubingwa wa dunia wa mbio za mita 800 za wanawake Berlin nchini Ujerumani. Kenya ilikata rufaa ikitilia shaka jinsi yake kutokana na maumbile yake yenye miraba minne.

Post a Comment

emo-but-icon

item