KADA WA CHADEMA MAREHEMU GERVAS KALOLO KUZIKWA LEO
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/kada-wa-chadema-marehemu-gervas-kalolo.html


Mbunge wa
Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) (katikati) akiwa na
baadhi ya waombolezaji nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa mashine tatu
mjini Iringa, mkoani Iringa leo mchana. (Picha na Friday Simbaya)

Baba
mdogo wa marehemu Gervas Kalolo, Mzee Raphael Kalolo (katikati) akitoa
maelezo mfupi ya marehemu kwa kwa mwandishi wa mjengwablog.com nyumbani
kwa marehemu katika mtaa wa mashine tatu mjini Iringa, mkoani iringa leo
mchana. (Picha na Friday Simbaya)




Katibu wa
Wilaya ya Iringa-Chadema, Suzana Mgonukulima (kulia) akitoa utaratibu
wa chama nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa mashine tatu mjini Iringa,
mkoani iringa leo mchana. (Picha na Friday Simbaya)

1. WASIFU WA MAREHEMU KUZALIWA
Marehemu GERVAS JOHN KALOLO alizaliwa tarehe 09.11.1964 katika Hospitali ya mkoa wa Iringa
2. ELIMU
Marehemu
GERVAS JOHN KALOLO alisoma shule ya awali na msingi katika shule ya
msingi CHEM CHEM hapa iringa mjini na kuhitimu mwaka 1980 na baadae
aliendelea na masomo ya Sekondari katika shule ya Sekondari HIGHLANDS
na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1983.
3. AJIRA
Mnamo
mwaka 1985 marehemu aliajiriwa katika kampuni ya IMAC ambako alifanya
kazi kwa muda mfupi. Na baadae aliacha kazi na kuamua kujishughulisha
na shughuli binafsi za Ujasiriamali na pia aliingia rasmi katika
shughuli za kisiasa.
4. UONGOZI KATIKA SIASA
Baada ya
kuingia katika siasa mnamo mwaka 2000 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa
mtaa.Na ilipofika mwaka 2005 alichaguliwa kuwa Mheshimiwa Diwani kupitia
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mpaka mwaka 2010. Mwaka huo huo
2010 aliamua kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na
mpaka umauti unamkuta alikuwa mmoja wa viongozi wa CHADEMA hapa
Iringa.
5. UONGOZI KATIKA KANISA
Marehemu GERVAS KALOLO alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Miyomboni Parokia ya Consolata – Mshindo.