FIGO: HISPANIA HAITABEBA KOMBE LA DUNIA MWAKA HUU, NADHANI BRAZIL WANASTAHILI
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/figo-hispania-haitabeba-kombe-la-dunia.html
NYOTA wa zamani wa kimataifa wa Ureno, Luis Figo amesema Hispania haitabeba kombe la dunia mwaka huu.
Figo
aliyeichezea Ureno mechi 125 na kufunga zaidi ya magoli 30 amesema
kikosi cha Vicente del Bosque hakina ubora wa kutetea ubingwa wao.
Hispania
imeshinda makombe makubwa matatu mfululizo kati ya mwaka 2008 na 2012,
japokuwa walipigwa na Brazil kwenye mechi Confederation Cup mwaka jana.
“Sidhani
kama Hispania watashinda kombe,” Figo aliuambai mtandao wa Laureus.com.
“ Sidhani kama wana ubora wa kufanya hivyo. Itakuwa vigumu kwao
kushinda, lakini sio kwamba haiwezekani”.
Badala yake Figo amewapa nafasi Brazil kutwaa ubingwa mwaka huu kwasababu wana kocha bora na faida ya kucheza nyumbani.
“Nadhani
inasaidia kucheza nyumbani. Namjua vizuri kocha wa Brazil (Luis Felipe
Scolari) na naamini ni kocha bora kwa mashindano kama haya na nchi
itaisaidia timu yao”. Aliongeza Figo.
“Itakuwa ngumu sana kwa timu zitakazocheza na Brazil ( kwasababu ya sapoti).”


Kiungo
huyo mstaafu alisema timu yake ya Ureno itahangaika sana kufika hatua
za juu za mashindano kwasababu inamtegemea zaidi Cristiano Ronaldo.
