Ubingwa: Yaya Toure akiwa ameshika kombe la ligi kuu na kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini.
YAYA
Toure amemuunga mkono wakala wake Dimitri Seluk aliyeishambulia
Manchester City baada ya kusahau sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na
kusema kuwa atatolea ufafanuzi wa hatima yake ya baadaye baada ya kombe
la dunia.
Seluk alisema hana uhakika kama nyota huyo wa Ivory Coast ataendelea kuwepo Etihad kwasababu hana furaha tena na klabu hiyo.
Yaya
ametweet: 'Wakala wangu alikuwa anajaribu kuweka wazi hoja ya msingi
kwa niaba yangu. Utani uwekwe pembeni. Inaonekana ni muhimu kwangu kutoa
tamko. Nitafanya hivyo".
"Kila alichokisema Dimitry ni sahihi. Ameongea kwa niaba yangu. Nitafanya mahojiano baada ya kombe la dunia ili kueleza".

Mapendekezo: Wakala wa Toure, Dimitri Seluk amesema kuna uwezekano mkubwa kwa nyota huyo kuondoka Etihad
Happy birthday to you! City waliandika kwenye mtandao wa Twita mei 13