BREAKING NEWS.WATU 17 WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI NIGERIA.
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/breaking-newswatu-17-wauawa-katika.html
Mji wa
Alagarno ambao uko katika jimbo la Borno, uko karibu na mji wa Chibok
ambako wasichana zaidi ya miambili walitekwa nyara na kundi la
wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram wiki tano zilizopita.
Juhudi
hizo zinawashikirisha wataalamu wa ujasusi wa kimataifa kutoka Israel,
Marekani na Uingereza.Hili ni shambulizi la hivi karibuni kufanywa
nchini Nigeria wakati nchi hiyo ikikumbwa na kitendawili cha kuwatafuta
zaidi ya wasichana miambili waliotekwa nyara na Boko Haram.
Pia
limetokea siku moja tu baada ya milipuko miwili kutokea mjini Jos katika
jimbo la Plateau ambapo takriban watu 118 waliuawa Jumanne usiku.
Juhudi za kuwatafuta maiti bado zinaendelea.
Mwandishi
wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa shambulizi lililofanyika mjini Jos,
lilisababishwa na Boko Haram na kwamba huenda ni ujumbe kwa serikali
kuwa wapiganaji hao wanaweza kushambulia wakati wowote wanapotaka.