FA YANOGESHA MAMBO!, WENGER KUPEWA MZIGO WA PAUNDI MILIONI 100 KUIMARISHA KIKOSI, KARIM BENZEMA, LARS BENDER WATUPIWA NYAVU
http://samchardtz.blogspot.com/2014/05/fa-yanogesha-mambo-wenger-kupewa-mzigo.html
Baada ya kutwaa ubingwa, Wenger amefanya maamuzi ya kubaki Emirates.
Alipoulizwa kama atasaini mkataba mpya mapema, alisema: "Ndiyo-kwasababu naenda Brazil juni 10".
Wenger
atapewa paundi milioni 100 kwa ajili ya usajili. Lengo lake la kwanza
ni kumshawishi beki wake wa pembeni Bacary Sagna na mlinda mlango,
Lukasz Fabianski ili wabakie klabuni hapo.
Pia anahitaji mshambuliaji mmoja wa kati, kiungo wa ukabaji na beki wa kulia.
Jembe
la kazi: Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema (katikati) ndiye
chaguo la kwanza kwa Arsenal katika usajili wa majira ya kiangazi.
Wenger pia anavutiwa na kiungo wa Bayer Leverkusen, Lars Bender (kulia)
