Makamu wa Rais apiga marufuku uharibifu wa mazingira nchini
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea katika...
https://samchardtz.blogspot.com/2016/11/makamu-wa-rais-apiga-marufuku-uharibifu.html
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepiga
marufuku uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea katika maeneo
mbalimbali nchini ambao unaweza kusababisha nchi kugeuka jangwa.
Makamu
wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kufungua mkutano wa kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia
ya nchi unaokutanisha wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini
ya Usimamizi wa Kigoda cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na
mabadiliko ya Tabia ya nchini katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais ameonya kuwa jukumu la kuhifadhi mazingira sio la Serikali peke
yake bali ni kila mwananchi na wadau wa mazingira kwa ujumla, hivyo
wananchi ni muhimu kwa umoja wao wakaongeza jitihada za kupanda miti
katika maeneo yao ili kukabiliana na hali tete ya uhabifu wa mazingira
nchini.
“Uharibifu wa mazingira usimame leo na marekebisho ya uharibifu tulioufanya uanze leo na hili ni jukumu la kila Mtanzania”
Makamu
wa Rais pia ametoa wito maalum kwa viongozi wa ngazi zote nchini
kuchukua hatua katika kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji katika maeneo
yao ili visitoweke.
Makamu
wa Rais ametahadharisha kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yameanza
kuleta athari si kwa Tanzania na dunia kwa ujumla hivyo jitihada za
makusudi zinahitajika ili kuhakikisha changamoto zinazojitokeza kwa sasa
zinakabiliwa ipasavyo.
Kwa
upande wake,Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya mabadiliko ya Tabia ya
nchi,Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Pius Yanda alisema mkutano huo
wa siku TANO utakuwa na jukumu kubwa la kujadili kwa kina namna bora ya
kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.