Flatnews

MGOGORO ZANZIBAR!..HAPATOSHI VIGOGO WENGINE 9 WAJIUZULU>>>>SOMA HAPA

                              Mawaziri sita wajiuzulu kutoka katika Chama cha upinzani CUF, mawaziri hao wamechukua hatua hiyo kutokana ...


                             
Mawaziri sita wajiuzulu kutoka katika Chama cha upinzani CUF, mawaziri hao wamechukua hatua hiyo kutokana na msuguano wa kisiasa visiwani humo.

Waziri wa sheria na katiba Abubakar Khamis Bakary alitoa kauli hiyo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya maazimio yaliyofikiwa na baraza la chama la Halmashauri kuu ya Taifa.

Mawaziri wengine waliojiuzulu ni Fatma Abdulhabibu Fereji,Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais wa kwanza, waziri wa Biashara, Viwanda na Makoso Nassor Ahmed Mazrui, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji, Waziri wa afya Rashidi Suleiman na Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdillah Jihadi.

Na wengine ni, Haji Mwandani Makame aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi na Nyumba, Maji na Nishati, Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo Zahara Ali Hamed na Naibu Waziri wa Kilimo Maliasili Mtumwa Kheir Mbarak.

Kwa mujibu wa Abubakary kila Waziri na Manaibu wao wamekabidhi magari ya serikali na vifaa vingine kwa mamlaka na kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha (28) ya katiba ya Zanzibar, umiliki wa ofisi kwa ajili ya wote akiwemo na Rais Dr Ali Mohamed Shein na mawaziri kumalizika Novemba 2.

Related

NEWS 7094037789141852754

Post a Comment

emo-but-icon

item