Flatnews

MESSI AUDHIHIRISHIA ULIMWENGU MWABA YEYE NI SUMU, BARCA YAISHUSHIA BALAA ROMA YA MAGOLI 6 - 1

Messi akicheza mchezo wake wa pili tangu aliporejea kutoka kwenye majeruhi ya muda mrefu ameisaidia timu ke kuibuka na ushindi wa magili ...


Messi akicheza mchezo wake wa pili tangu aliporejea kutoka kwenye majeruhi ya muda mrefu ameisaidia timu ke kuibuka na ushindi wa magili 6-1 dhidi ya AS Roma kwenye mchezo wa kundi E
wa michuano ya UEFA Champions ligi uliochezwa usiku wa Jumanne November 24 kwenye uwanja wa nyumbani wa Barcelona Nou Camp.
Akiwa katika kiwango cha hali ya juu Messi alifanikiwa kutupia kambani goli mbili kwenye ushindi wa sita huku akisaidia kupatikana kwa magoli mengine. Messi alicheza kwa dakika zote 90 za mchezo dhidi ya Roma.
                                  Barca 1
Ghalika ya magoli ilianza kuishukia Roma mapema kipindi cha kwanza baada ya Luis Suarez kufunga goli la kuongoza dakika ya 15 ya kipindi cha kwanza, dakika tatu baada Lionel Messi akaifungia Barcelona goli la pili kabla ya Suarez hajaongea bao la tatu dakika ya 44 na kuifanya Barcelona kwenda mapumziko ikiwa kifua mbele kwa mabao 3-0.
Mvua ya magoli ilizidi kuiandama Roma kipindi cha pili baada ya beki wa Barcelona Gerrard Pique kupachika bao la nne dakika ya 56 huku Messi akirejea tena nyavuni dakika ya 60 na Adriano akahitimisha ushindi kwa kufunga goli la sita dakika ya 77.
                                Barca 2
Nyota wa Brazil na Barcelona Neymar yeye aliosa penati 77 na kushindwa kufunga goli na kuwa mchezaji pekee ambaye hakufunga goli kwenye umoja wa washambuliaji wa Barca (mapacha watatu).
Mshambuliaji wa AS Roma Edin Dzeko aliifungia timu yake bao pekee kwenye kipigo hicho ilichokipata timu yake huku akipoteza mkwaju wa penati ilioupata timu yake dakika ya 82.

Related

SPORTS 6021336050010571966

Post a Comment

emo-but-icon

item