Flatnews

Lowassa Kuzungumza na Watanzania Kuhusu Uchaguzi Zanzibar na Msimamo wake Baada ya Magufuli Kutangazwa Mshindi

Aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, ameibuka na mambo mengi mazito kuhusia...



Aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, ameibuka na mambo mengi mazito kuhusiana na kile kilichotokea katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 na kumuweka madarakani Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli.

Taarifa kutoka ndani ya muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambavyo Lowassa alikuwa akiviwakilisha kwa nafasi ya urais vya Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD, inaeleza kuwa Lowassa atafichua kila kitu kuhusiana na uchaguzi huo wakati atakapozungumza jijini Dar es Salaam leo na vyombo vya habari  vya ndani na vya kimataifa.

Kadhalika, taarifa hiyo inaeleza kuwa mbali na kufichua mazito kuhusiana na uchaguzi mkuu ambao yeye alitangazwa kuwa mshindi wa pili bada ya kupata asilimia 39.97 ya kura halali zilizopigwa na kuachwa na Dk. Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyepata asilimia 58.46, Lowassa pia atashirikiana na viongozi wa Ukawa kuelezea msimamo wao kuhusu uchaguzi uliofutwa wa Zanzibar ambao mgombea urais wa CUF na Ukawa, Maalim Seif Sharif Hamad, anadaiwa alikuwa akielekea kushinda.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, ndiye aliyeufuta uchaguzi wa Zanzibar siku tatu baada ya kufanyika kwake kutokana na kile alichoeleza kuwa ni kuwapo kwa kasoro nyingi zilizoufanya uchaguzi huo usiwe ‘huru na wa haki’.

Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu jana, Msemaji wa Lowassa, Aboubakar Liongo, alisema Lowassa atazungumza leo jijini Dar es Salaam na kueleza mengi kuhusiana na kilichotokea katika uchaguzi mkuu, akiwa pamoja na viongozi wengine wa Ukawa akiwamo Maalim Seif.

“Lowassa atazungumza katika mkutano huo… pia Maalim Seif anatarajiwa kuwapo. Atazungumzia msimamo wa Ukawa juu ya hali ya Zanzibar na kutoa kauli nini kinafuata baada ya kuporwa ushindi,” ilisema sehemu ya taarifa iliyotolewa na Liongo jana.

Aidha, akizungumza jana, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Profesa Abdallah Safari, aliwaambia wananchi kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea ubunge wa chama chao jijini Arusha, Godbless Lema, kuwa Lowassa ana mengi mazito kuhusiana na uchaguzi mkuu ambayo atayatoa leo mbele ya waandishi wa habari wa ndani na wa kimataifa. 
 
Aliyasema hayo kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro.

Alisema tofauti na walivyopanga awali kuwa Lowassa ahudhuhurie mkutano huo wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi wa Jimbo la Arusha Mjini, sasa atafanya hivyo wakati wa kufunga kampeni kwani jana hiyo alikuwa katika maandalizi ya kuzungumza na waandishi, hasa kuhusiana na hujuma zilizofanyika katika uchaguzi mkuu uliopita.

“Mnaelewa jinsi kura zake zilivyoibiwa… sasa kesho (leo) atazungumza na waandishi wa habari wa ndani na nje kuhusu kadhia hiyo,” alisema Profesa Safari na kuongeza: “Sasa atakuja siku ya mwisho ya kufunga kampeni kumnadi Lema.”

Kuhusu Zanzibar
Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Twaha Taslima, ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, alisema kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar ni suala ambalo limewashitua wengi wengi nchini na duniani kwani ni kukiukwa wazi wazi kwa misingi ya demokrasia.

“Uchaguzi mpya Zanzibar siyo sawa… na kila mtu anaona hiyo si sawa, lakini tunashangaa kuona uchaguzi unarudiwa. Viongozi wetu wapo na watawaambia cha kufanya,” alisema Taslima.

“Hali inayoendelea Zanzibar inatia doa sura ya Tanzania katika uso wa Dunia. Mimi ni mmoja wa viongozi hao, tunajiandaa kutoa tamko kesho (leo),” aliongeza Taslima, akikumbushia uchaguzi uliofutwa Zanzibar ambao mgombea wa CUF na Ukawa, Maalim Seif, aliwaambia waandishi wa habari kabla ya kufutwa kwa uchaguzi huo kwamba alikuwa akiongoza kwa asilimia 52.87 kutokana na karatasi za matokeo walizokusanya kutoka katika vituo vyote vya uchaguzi visiwani Zanzibar.

Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema ukimya wa Watanzania usiwafanye watwala kuamini kuwa wao (Ukawa) ni ‘wapumbavu na malofa’ kama alivyowatuhumus Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati wa kampeni za uchaguzi na badala yake wanatakiwa kuzingtia sheria na kutenda haki.

Related

NEWS 3565793456486122009

Post a Comment

emo-but-icon

item