Flatnews

KUELEKEA MCHEZO WA MADRID VS BARCELONA, HIVI NI VITU VITANO USIVYOVIJUA KUHUSU MCHEZO WA EL CLASICO

  Real Madrid na Barcelona zitaumana kwenye mchezo wao wa ligi maarufu kama El Clasico utakaochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu ...


 Real Madrid na Barcelona zitaumana kwenye mchezo wao wa ligi maarufu kama El Clasico utakaochezwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu Jumamosi ya November 21, katika historia ya mchezo huo Real Madrid maarufu kama Los Blncos wao ndio wanaongoza kushinda idadi ya mechi nyingi wakiwa wameshinda michezo 92 wakati Barelona wao wakiwa wameshinda mechi 89.

Kabla hujakaa chini kuangalia mchezo huo siku ya Jumamosi, inawezekana kuna baadhidi ya vitu ambavyo huvifahamu kuhusu mchezo huo mkubwa kwenye historia ya soka.
  1. Ushindi mkubwa kwenyehistoria ya mchezo wa El Clasico
Real Madrid 11-1 Barcelona (13 June 1943)
Magoli Madrid vs BarcaKwenye msimu wa mwaka 1943, Barcelona iliifunga Real Madrid magoli 3-0 nyumbani kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya kombe la Copa del Rey, lakini kikosi cha Real Madrid kilionesha kiwango kizuri kuwahi kutokea kwenye mchezo wa soka na kufanikiwa kuifunga Barcelona bao 11-1 kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu kwenye mchezo wa marudiano na kutinga hatua ya fainali ya kombe hilo.
  1. Kipindi kirefu bila kupoteza mchezo wa El Clasico
Barcelona: Mechi 13 (1 November 1917- 3 June 1928)
Madrid vs Barca 2
Barcelona iliweza kucheza kwa miaka 11 bila kupoteza mchezo dhidi ya Real Madrid kwenye mashindano yote kuanzia November 1, 1917 hadi June 3, 1928, watoto wa Catalan pia wanashikilia rekodi ya kukaa muda mrefu zaidi bila kufungwa kwenye mchezo wa El Clasico kwenye ligi (La Liga) ikiwa hawajapoteza michezo saba, kuanzia December 2008 hadi December 2011 wakifanikiwa kushinda michezo sita kati ya saba.
  1. Mfungaji bora wa muda wote kwenye El Clasico
Lionel Messi: Magoli 21
Madrid vs Barca 3
Lionel Messi ndiye mcheaji anayeongoza kutupia kambani kwenye mechi ya El Clasico akiwa kafunga magoli 21 kwenye michezo 30 aliyocheza. Magoli 14 kwenye mechi za ligi (anafungana na Di Stefano), amefunga magoli matano kwenye michuano ya Super Cup na magoli mawili kwenye UEFA Champions League.
  1. Rekodi ya Kufunga mfululizo kwenye El Clasico
Madrid vs Barca 4
Cristiano Ronaldo: Mechi 6
Cristiano Ronaldo anashikilia rekodi ya mchezaji ambaye amefunga mfululizo kwenye mechi za El Clasio akiwa amefunga magoli 7 kwenye mechi 6 zilizopita tangu 2011-2012 Copa del Rey (mechi ya raundi ya kwanza) hadi 2012-13 mechi ya La Liga.
  1. Nidhamu mbovu kwenye mechi za El Clasico
Fernando Hierro: Kadi 19
Madrid vs Barca 5Mchezaji wa zamani na nahodha wa Real Madrid Fernando Hierro anaonekana kama mchezaji mwenye nidhambu mbovu kuwahi kutokea kwenye historia ya mechi za El Clasico akiwa amepewa jumla ya kadi 19 kwenye historia ya mchezo huo. Kati ya kadi hizo, 18 ni za njano huku moja ikiwa ni nyekundu.
Ramosi anaongoza kupewa kadi kwa wachezaji wa sasa, ameshaoneshwa kadi 16 (kadi 14 za njano na nyekundu mbili.

Related

SPORTS 7473092107201379256

Post a Comment

emo-but-icon

item