Flatnews

Job Ndugai: Tutegemee Migomo Katika Bunge Hili la 11

Baada ya kuteuliwa na CCM na kupita katika mchakato wa kumpata mgombea Uspika wa Bunge la Kumi na moja bila kupingwa, Job Nduga...


Baada ya kuteuliwa na CCM na kupita katika mchakato wa kumpata mgombea Uspika wa Bunge la Kumi na moja bila kupingwa, Job Ndugai ameeleza changamoto anazotarajia kukutana nazo ikiwa ni pamoja na migomo.

Akiongea na waandishi wa habari jana baada ya jina lake kupitishwa, Ndugai alilielezea Bunge la kumi na moja kama Bunge lenye utofauti mkubwa na mabunge mengine huku akidai kuwa ongozeko la vijana wengi na wasomi wengi zaidi kunaashiria kuongezeka kwa changamoto zaidi.

“Bunge hili lina wabunge wengi vijana, lina wabunge wengi wasomi zaidi kuliko mabunge yote yaliyowahi kutokea na lina uwakilishi mkubwa. Hili ni Bunge ambalo litakuwa na changamoto nyingi, tetegemee migomo ya hapa na pale, hata hivyo ubora wa kazi utakuwa mkubwa,” alisema Ndugai.

Hata hivyo, Ndugai alisisisitiza kuwa ataliongoza Bunge kwa weledi na kutenda haki kwa kila upande hivyo aliwataka wabunge wote wakiwemo wa upinzani kumuunga mkono leo ili awe Spika wa Bunge la 11.

Related

NEWS 7834045090503244782

Post a Comment

emo-but-icon

item