SUALA LA YULE DAKTARI WA CHELSEA, MOURINHO PRESHA INAPANDA NA KUSHUKA
Presha imezidi kuwa kubwa kwa kocha Jose Mourinho wa Chelsea mara baada ya daktari Eva Carneiro kutoweka klabuni na sasa anawasiliana na...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/09/suala-la-yule-daktari-wa-chelsea.html
Presha imezidi kuwa kubwa kwa kocha Jose Mourinho wa Chelsea mara baada ya daktari Eva Carneiro kutoweka klabuni na sasa anawasiliana na wanasheria wakubwa kumsaidia kudai haki zake.
Eva na Mourinho waliingia katika
mzozo siku ya tarehe 8 mwezi uliopita katika mchezo wa sare ya bao 2-2
dhidi ya Swansea, baada ya Mourinho kumshutumu Eva kuwa sababu ya wao
kutopata ushindi katika mechi hiyo kwa kuwa alienda uwanjani kumtibia
Eden Hazard.
Baada ya Mourinho kumuadhibu
mwanadada huyo kwa kumkataza kukaa katika benchi la Chelsea, lakini pia
kutofika hotelini, mwadada huyo mwenye asili ya Gibraltar aliondoka
klabuni hapo na sasa amegoma kurudi tena kikosini kwa madai yakutoweza
tena kufanya kazi na Mourinho.
Imeelezwa kuwa kocha Jose
Mourinho alitoa kauli za matusi na ubaguzi baada ya kumtamkia dada huyo
maneno ya lugha chafu akizungumza kwa kireno na sasa dada huyo baada ya
kutopata sapoti ya klabu, ameamua kuikacha klabu hiyo na kutafuta haki
mahali kutako stahiki.
Mourinho anaweza kuwa matatani
baada ya FA kupata ushahidi wa kauli hizo za kibaguzi za Mourinho huku
pia chama cha madaktari nchini England kikitaka FA ichukue hatua.