PICHA ZA CRISTIANO RONALDO AKIZINDUA PERFUME YAKE “LEGACY”
Cristiano Ronaldo big brand kwenye soka anaendelea kufungua njia za kupiga pesa kwenye njia mbalimbali. Lakini biashara zake zote za...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/09/picha-za-cristiano-ronaldo-akizindua.html
Cristiano Ronaldo big brand kwenye soka anaendelea kufungua njia za kupiga pesa kwenye njia mbalimbali. Lakini biashara zake zote za nje zinatokana na perfomance yake ya mchezoni ndio
maana haachi kusema kwamba lazima acheze vizuri uwanjani hicho ndicho kitu chake cha kwanza.
Hivi sasa Ronaldo amezindua perfume yake mpya ambayo ameipa jina la Legacy. Kwenye maelezo yake anasema huwa anatumia kila siku perfume kwenye maisha ya kawaida, hivyo basi alitaka kuwa na ile moja anayoitamani kwa jina lake. Pia anajaribu kuwapa mashabiki zake kila kitu ambacho yeye anakipenda. Kuanzia mashati, viatu, perfume hadi suti.
