STARS YAANZA MAZOEZI BILA WAKALI ‘KIBAO’…
Kikosi cha tiu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo asubuhi kimeanza mazoezi ya kujiandaa na pambano la kuwania kufuzu kucheza michua...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/08/stars-yaanza-mazoezi-bila-wakali-kibao.html
Kikosi
cha tiu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo asubuhi kimeanza
mazoezi ya kujiandaa na pambano la kuwania kufuzu kucheza michuano ya
Mataifa ya Afrika (CHAN) dhidi ya timu ya Nigeria mchezo unaotarajiwa
kuchezwa Septemba 5, kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kikosi
kilichofanya mazoezi siku ya leo ni sehemu ndogo ya timu nzima ya Taifa
kwasababu wachezaji wengi wa timu za Yanga na Azam wamezuiwa kujiunga
na timu hiyo kutokana na kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii ambayo
itapigwa Agosti 22 mwaka huu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu
msimu wa 2015-2016.
Wachezaji
ambao wapo kambini mpaka sasa ni 17 lakini awali kocha mkuu wa timu
hiyo Charles Boniface Mkwasa alitangaza kikosi cha wachezaji 29 ambacho
kilitakiwa kuingia kambini. Wachezaji wa kimatafa wao watawasili baadae
kwasababu ruhusa yao kutoka kwenye vilabu vyao kwenda kwenye timu za
taifa inatokana na kalenda ya FIFA.
Kutokana
na Yanga pamoja na Azam kuzuia wachezaji wao wakijiandaa na mechi ya
Ngao ya Jamii, MKwasa amelazimika kuwaita wachezaji wengine 10 ili
kujaribu kuziba nafasi za wachezaji wengine ambao bado hawajaripoti.
Wachezaji walioongezwa kwenye
kikosi cha Stars ni Mohamed Yusufu (Tanzania Prisons), Sid Mohame (Mibwa
Sugar), Vicent Andrew (Mtibwa Sugar), Mohamed Hussein ‘Tshabalala’,
(Simba SC), Ibrahim Ajibu (Simba SC), Hamisi Ally (KMKM), Juma Mbwana
(KMKM), Tumba Swed (Coastal Union), Samwel Kamuntu (JKT Ruvu) na Ibrahim
Hilka (Zimamoto-Zanziabar) .
