SIMBA MKALI LAKINI ANAZAA..! HATA MAREFA NAO WANA TIMU ZAO LICHA YA KUWA ‘MAKAUZU’ UWANJANI
Asalam aleykum wapenzi wa michezo popote mnapoisoma Makala hii, naamini hali zenu ni nzuri na mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/08/simba-mkali-lakini-anazaa-hata-marefa.html
Asalam aleykum wapenzi wa michezo
popote mnapoisoma Makala hii, naamini hali zenu ni nzuri na mnaendelea
vyema na shughuli zenu za kila siku. Baada ya kuwa bize na habari za
siasa ambazo ndizo zinasumbua vichwa vya watu kibao, naomba sasa utulie
na uburudike na habari moto moto za kimichezo katika ukurasa huu ambao
pengine ndio unaoongoza kwa kusomwa na wapenzi wengi wa soka nchini
Tanzania.
Kila binadamu mpenzi wa soka lazima ana timu anayoipenda kwa dhati, huwezi kuwa mpenda soka alafu ukakosa timu ya kuishabikia, bila shaka wewe utakuwa ‘Lofa’ kama sio Mnafiki. Mimi binafsi mbali na kuipenda
timu yangu ya nyumbani ya AFC ya hapa Arusha, pia ni shabiki wa kutupwa wa Borussia Dortmund na ninaumia sana tunapoonewa na wale wekundu wa Munich, anyway waamuzi wa soka pale EPL pia wamekuwa
wakichezesha mechi kibao ila nao kama binadamu na wapenzi wa soka wana vilabu vyao.
Leo hii naomba upoteze muda wako kutazama baadhi ya waamuzi na taaluma zao nje ya uwanja huku nikikuwekea pia na timu wanazozipenda kutoka moyoni licha ya kufanya kazi za Uamuzi, karibu sana tafadhali.
MARK CLATTENBURG- SHABIKI WA KUTUPWA WA NEWCASTLE UNITED
Mark Clattenburg
Ni mwamuzi mwenye miaka 40 na anakuwa miongoni mwa waamuzi
wadogo kabisa kwenye EPL. Ndani ya misimu mitatu iliyopita amesha
chezesha mechi 75 na kutoa kadi za njano 258 huku nyekundu zikiwa 11.
Alianza kazi yake akiwa na miaka 25, nadhani wengi tutamkumbuka kwa ile
kashfa ya kumbagua Mikel Obi kwenye mechi ya EPL japokuwa baadae
alikutwa hana hatia. Aliweka rekodi kwa kuwa mwamuzi mdogo kuchezesha
mechi za FIFA, hapa alikuwa na miaka 30.
Kitaaluma huyu mwamuzi ni Mwanasheria ila hapo awali alikuwa
ni fundi umeme. Kama alivyo mwanadamu mwingine, Clattenburg pia ana
hisia na kuguswa na timu fulani. Hapa nazungumzia mapenzi yake kwenye
timu ya Newcastle Unted. Mwamuzi huyu amekuwa akiguswa na uchezaji wa
Newcastle tangu siku nyingi na amekiri mara kadhaa.MARTIN ATKINSON- SHABIKI WA KWELI WA LEEDS UNITED
Martin Atkinson
Huyu jamaa ana miaka 44 na
alianza kazi ya uamuzi pindi akiwa na miaka 16, kazi hii aliianza baada
ya kutokuwepo kwa waamuzi kwenye mechi za mtaani kwake. Tunamfahamu
zaidi kwa uamuzi wake wa furaha kwani jamaa anaweza kukupa kadi huku
anacheka. Hadi sasa ndani ya misimu mitatu iliyopita Martin amechezesha
mechi 82 na kutoa kadi za njano 294 huku kadi nyekundu zikiwa 11. Amesha
chezesha mechi kubwa sana katika ngazi zote za vilabu barani Ulaya.
Kitaaluma huyu jamaa ni Polisi, ndiyo nakwambia ni afisa wa
Polisi sasa unashangaa nini..! Japokuwa alionekana kuipendelea Man U,
ila huyu jamaa ni mpenzi na shabiki mkubwa wa Leeds United ya paleUingereza. Amekuwa akivurunda mara kibao na pia mara chache ameomba radhi kwa madudu yake uwanjani.
ANTHONY TAYLOR- SHABIKI WA KUFA WA ALTRINGHAM FC
Anthony Taylor
Japokuwa ana miaka 36, ila
alianza kazi ya uamuzi muda mrefu sana tangu wakati Rais mkapa anaingia
madarakani. Kaanza kazi siku nyingi sana ila alipandishwa kuchezesha
ligi kuu mwaka 2010 kwani muda mwingi alikuwa anachezesha mechi za
madaraja ya chini huko Uingereza. Ndani ya misimu mitatu iliyopita
ameshachezesha mechi 74 na kumwaga kadi 237 huku akitoa kadi nyekundu 13
pekee. Taylor amekuwa miongoni mwa waamuzi wanaolalamikiwa mara kwa
mara.
Taaluma yake ni bwana jela. Eeeh, bwana jela ndiyo sasa
unashangaa kitu gani..! Mbali na kufanya kazi na wafungwa, pia huyu
jamaa ni shabiki wa kufa wa timu ya Altringham FC, timu kongwe
inayopatika hukoManchester na inashiriki madaraja ya chini. Watu wengi tunamkumbuka zaidi alipovurunda mechi ya Arsenal na Aston Villa mwaka 2013.
MIKE DEAN- SHABIKI HATARI WA TRANMERE ROVERS.
Mike Dean
Ni miongoni mwa waamuzi wakongwe
kabisa barani Ulaya na nchini Uingereza akiwa na miaka 47 hadi sasa.
Mike anadai yeye ni mkongwe kwenye fani hii kwani ana miaka 30 tangu
aanze kuchezesha mechi za
soka. Ukijaribu kuangalia misimu mitatu iliyopita, Mike amechezesha mechi 84 huku akimwaga kadi za njano kama njugu kwa kutoa jumla ya kadi 322 na zile nyekundu 15 pia. Mike alitajwa mara kadhaa kustaafu tangu
akiwa na miaka 45 ila cha ajabu bado yupo dimbani.
Japokuwa taaluma yake amekuwa akiificha, ila ukweli ni
kwamba Mike ni shabiki wa kufa wa Tranmere Rovers. Timu hii ni kongwe
sana kwani ina miaka mingi na imekuwa ikishiriki madaraja ya chini ya
ligi zasoka. Ukijaribu kuangalia misimu mitatu iliyopita, Mike amechezesha mechi 84 huku akimwaga kadi za njano kama njugu kwa kutoa jumla ya kadi 322 na zile nyekundu 15 pia. Mike alitajwa mara kadhaa kustaafu tangu
akiwa na miaka 45 ila cha ajabu bado yupo dimbani.
Uingereza. Anakumbukwa zaidi kwa kumuogopa Ferguson kwani mwaka 2010 aliwanyima Chelsea penati 4 Old Trafford.
MICHAEL OLIVER- SHABIKI WA KUTUPWA WA NEWCASTLE UNITED.
Michael Oliver
Ni mwamuzi mdogo pengine kuliko
wote kwa sasa katika ligi kuu ya Uingereza. Oliver ana miaka 30 pekee na
ameanza kazi yake tangu akiwa na miaka 14. Bwana mdogo huyu amekuwa
gumzo sana kwani ndani ya misimu mitatu iliyopita, ameshachezesha mechi
77 na kutoa kadi za njano 248 huku zile nyekundu zikiwa 8. Anashikilia
rekodi ya kuwa mwamuzi mdogo kuchezesha EPL akiwa na miaka 25 mwaka
2010. Bila shaka unamfahamu zaidi huyu jamaa kwani tushaandika Makala
sana kumuhusu.
Nje ya uwanja huyu Jamaa anafanya kazi ya kuratibu waamuzi
kwenye akademi inayofunza waamuzi. Pia ni shabiki wa kutupwa wa
Newcastle na hii inachagizwa na kukulia kwake karibu na timu hii. Bila
shaka wengiwanamkumbuka kwenye mechi ya Chelsea na Swansea na alivyompa Di Maria
kadi nyekundu.
LEE MASON- MNAZI WA BOLTON WANDERERS
Lee Mason
Ni Babu Fulani mwenye kipara na
mwaka huu anatimiza miaka 43 tangu kuzaliwa kwake. Ni miongoni mwa
waamuzi wachache walioanza kazi kabla hata Michael Oliver hajazaliwa..!
Ana wastani wa kutoa kadi tatu za njano kwa kila mechi kwani tayari
ametoa kadi 225 ndani ya mechi 73 hadi
sasa huku akiwa na kadi 12 nyekundu katika vitabu vya rekodi. Mwaka 2006 Mason alichezesha mechi yake ya kwanza ya EPL na baada ya hapo amekuwa na mwendelezo wa kuchezesha mechi kibao.
Nje ya soka, Lee Mason ni Mfanyabiashara na kabla ya hapo
alikuwa ni mkusanya kodi nchini Uingereza. Kama walivyo binadamu
wengine, Masoni pia ana mapenzi na timu fulani, timu hii siyo nyingine
bali ni Boltonsasa huku akiwa na kadi 12 nyekundu katika vitabu vya rekodi. Mwaka 2006 Mason alichezesha mechi yake ya kwanza ya EPL na baada ya hapo amekuwa na mwendelezo wa kuchezesha mechi kibao.
Wanderers. Mwamuzi huyu anakumbukwa kwa kuwaonea Chelsea mwaka 2012 pale alipowatoa nje Torres na Ivanovic huku akiwanyima Blues penati kadhaa pale Old Trafford.
