Rais Kikwete aongoza Kikao Cha Halmashauri Kuu mjini Dodoma leo
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu Mwenyekiti Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu ...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/08/rais-kikwete-aongoza-kikao-cha.html

Mwenyekiti
wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu Mwenyekiti Zanzibar
Dkt.Ali Mohamed Shein,Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Philip Mangula na
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakipiga makofi pamoja na
wajumbe wengine muda mfupi baada ya kuingia katika ukumbi wa White House
Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma tayari kuendesha kikao cha Halmashauri
Kuu ya CCM leo jioni.

Wajumbe
wa Halmashauri kuu ya CCM Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete na Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha
wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Halmashauri kuu
ya CCM mjini Dodoma leo.

Waziri
Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni mgombea wa Urais
kwa tiketi ya CCM Dkt.John Pombe Magufuli wakiteta muda mfupi kabla ya
kuanza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma leo.
Picha na Freddy Maro.