MURO, JULIO, MATOKEO YAO YA UBUNGE NA UDIWANI HAYA HAPA…
Kocha wa Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameangukia pua kwenye kura za maoni kuwania kuteuliwa kuwania nafasi ya Udiwani...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/08/muro-julio-matokeo-yao-ya-ubunge-na.html
Kocha
wa Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameangukia pua kwenye
kura za maoni kuwania kuteuliwa kuwania nafasi ya Udiwani wa kata ya
Kigogo kupitia Chama Cha Mapinduzi baada ya kumaliza akiwa nafasi ya
tatu kwenye kinyang’anyiro hicho.
“Nimemaliza mtu wa tatu katika
kura za maoni kata ya Kigogo na hiyo siyo maana nimeshindwa kwasababu
kawaida ya CCM baada ya kura za maoni majina yanapelekwa Wilayani na
baadae Mkoani ili kupitia jina la kila mmoja ili kuona yupi anafaaili
aweze kwenda lakini kwa jinsi ambavyo Julio Alberto sikufanya kampeni za
kupita nyumba kwa nyumba kwasababu mimi sera yangu sitaki rushwa”.
Wanamichezo
wengine walioangukia pua kwenye kura za maoni ni pamoja na Afisa habari
wa Yanga Jerry Muro na Abdalla Idirisa Majura waliokuwa wakiwania
kuteuliwa na chama chao kuwania Ubunge wa jimbo la Kawe.
