WAAMUZI WA KAGAME KUPIGWA ‘MSASA’ KESHO
Baraza la Vyama Vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kesho Alhamisi Julai 16, litaendesha mtihani wa utimamu wa mwili...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/07/matokeo-ya-ualimu-2015-nayo-yako-hewani.html
Baraza
la Vyama Vya Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kesho
Alhamisi Julai 16, litaendesha mtihani wa utimamu wa mwili (Physical
test) kwa waamuzi wa
watakochezesha michuano ya kombe la Kagame
inayoanza mwishoni mwa wiki huu.
Zoezi
hilo la utimamu kwa waamuzi watakochezesha mashindano ya Kagame,
litafanyika kuanzia saa 2 asubuhi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam litasimamiwa na kamati ya waamuzi ya ya CECAFA.
Waamuzi
wanaotarajiwa kuhudhuria zoezi hilo ni Ali Ahmed, Suleiman Bashir
(Somalia), Ahmed Djama (Djibout), Yetayew Belachew (Ethiopia), Kakunze
Herve (Burundi), Davis Omweno, Peter Sabata (Kenya), Issa Kagabo,
Hakizimana Louis (Rwanda), Ahemd El Faith (Sudan), Lee Okelo na Mashood
Ssali (Uganda), Israel Mjuni na Ferdinand Chacha (Tanzania).