Chadema yapangua ratiba fomu za ubunge, udiwani
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelazimika kupangua ratiba ya awali ya uchukuaji fomu za ubunge na udiwani kwa wa...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/07/chadema-yapangua-ratiba-fomu-za-ubunge.html

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelazimika kupangua ratiba ya awali ya uchukuaji fomu za ubunge na udiwani kwa wanachama wake, baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza majimbo mapya 26 ya uchaguzi hivi karibuni.
Aidha, kimeruhusu wanachama wote wenye sifa kuchukua na kurejesha
fomu za kuwania uteuzi wa ndani ya chama katika nafasi za udiwani na
ubunge katika majimbo yote ya uchaguzi nchi nzima.
Kupitia Waraka wa Katibu Mkuu Namba 5 wa mwaka 2015 uliosainiwa na
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa, wananchi wenye nia na
sifa za kuchukua fomu za ubunge kwenye majimbo yote yakiwemo mapya
wanaruhusiwa kufanya hivyo hadi keshokutwa Jumapili.
Kwa mujibu wa Dk Slaa, kwa nafasi za udiwani, uchukuaji na urejeshaji
wa fomu katika kata zote nchi nzima limeongezwa muda hadi Julai 29.
Alisema awali Chadema ilitoa ratiba yake ya uteuzi wa ndani ambapo
ilionesha kuwa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania udiwani na
ubunge katika kata na majimbo yenye madiwani au wabunge wa chama hicho
ulitakiwa kusubiri hadi halmashauri zitakapokoma.