TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 96
TAREHE 12 JUNI, 2015 MEYA MWANZA KUFUNGA U13 KESHO Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kesho jumamosi atafunga ras...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/06/taarifa-kwa-vyombo-vya-habari-release.html
TAREHE 12 JUNI, 2015
MEYA MWANZA KUFUNGA U13 KESHO
Mstahiki
Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kesho jumamosi atafunga rasmi
mashindano ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 13.
Sherehe ya kufunga mashindano hayo itafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia majira ya saa9 kamili alasiri .
Kwa takribani wiki moja sasa mashindano hayo yamekuea yakiendelea jijini Mwanza katika viwanja vya Alliance na CCM Kirumba.
Lengo
la mashindano haya ni kuibua vipaji kwa ajili ya kupata timu ya Taifa ya
awali itakayojiandaa na fainali za vijana Afrika wenye umri chini ya
miaka 17 mwaka 2019 fainali zitafakazonyika nchini Tanzania.
Katika
kutambua na kujiunga na watanzania wenzetu wenye ulemavu wa ngozi
(Albino) siku hiyo ya tareje 13/06/2015, TFF itajiunga na familia ya
walemavu wa ngozi katika kuadhimisha siku yao kimataifa na kuonyesha
bango maalum leney kuelimisha umma juu ya ubaya wa uovu wa kuwaumiza na
kuwaua wenzetu wenye ulemavu wa ngozi.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF).