Bayport yasogeza mbele ofa ya viwanja vya mikopo Vikuruti
Bayport yasogeza mbele ofa ya viwanja vya mikopo Vikuruti Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financ...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/06/bayport-yasogeza-mbele-ofa-ya-viwanja.html
Bayport yasogeza mbele ofa ya viwanja vya mikopo Vikuruti
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI
ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya
mikopo imesogeza mbele huduma yao mpya ya mikopo ya viwanja vilivyopo
Vikukuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa ajili ya kutoa fursa zaidi
ya Watanzania kupata viwanja hivyo vilivyopimwa.
Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial
Services, Ngula Cheyo, kushoto, akizungumza jambo baada ya kutangaza
kusogeza mbele huduma ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, wilayani
Kibaha, mkoani Pwani, ambapo sasa huduma hiyo imepelekwa mbele hadi Juni
30, mwaka huu. Picha na Mpiga Picha wetu.
Awali
ofa ya huduma hiyo ilipangwa kumalizika Juni 10 mwaka huu, lakini sasa
imepelekwa mbele hadi Juni 30, ikiwa ni ongezeko la siku 20 zaidi kama
njia ya kuhakikisha kwamba wale wenye nia hiyo wanafanikisha ndoto zao
za kumiliki viwanja.
Meneja
Biashara wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Thabit
Mndeme, kulia akizungumza jambo baada ya kutangaza kusogeza mbele huduma
ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani,
ambapo sasa huduma hiyo imepelekwa mbele hadi Juni 30, mwaka huu. Picha
na Mpiga Picha wetu.
Akizungumza
leo mchana jijini Dar es Salaam, Meneja Biashara wa Bayport Financial
Services, Thabit Mndeme, alisema kwamba wamekuwa wakipokea maombi mengi
kutoka kwa Watanzania wenye uhitaji wa viwanja hivyo, jambo
lililowafanya wakae na kuona namna gani wataongeza siku chache kwa
wananchi na wateja wao. Alisema kama ilivyokuwa mwanzo, wateja wao
watalazimika kuchukua fomu za maombi ya mikopo ya viwanja hivyo katika
ofisi yoyote ya Bayport, bila kusahau wakala wao ambayo ni tawi lolote
la Bank of Africa (BOA), huku akitakiwa kulipa malipo ya awali kuanzia
Sh 150,000.
“Kama
ilivyokuwa mwanzo, mara baada ya mteja wetu kuchukua fomu na kulipa Sh
150,000 kwa kupitia benki ya BOA, ataleta nyaraka zake kwetu na
atapatiwa kiwanja chake, huku gharama za kiwanja cha chini kabisa ni Sh
1,400,000, ambapo Bayport itamlipia gharama zilizosalia, huku
akilazimika kulipia Sh 105,181 kwa mwezi kwa kipindi cha miezi 24,”
alisema Mndeme.
Naye
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo,
alisema kwamba huduma yao ni muhimu kwa watumishi wa umma, wafanyakazi
wa kampuni binafsi na wajasiriamali ambao wote kwa pamoja wanachotakiwa
kufanya ni kuchukua fomu na kuchagua viwanja watakavyo, kutoka kwenye
mradi huo wenye viwanja 1878, huku pia mteja akiweza kupata kiwanja kwa
fedha taslimu ya kuanzia Sh 1,400,000 na kuendelea.
“Viwanja
hivyo vina uwezo wa kujengwa nyumba za kupanga na kupangisha, hoteli na
maduka, vituo vya elimu na ibada, hospitali na kumbi mbalimbali, huku
mradi wa umeme na maji vikiwa vinapatikana ndani ya mradi huo ambao ni
kilomita 50 kutoka Kisutu jijini Dar es Salaam na kilomita 6.5 kutoka
barabara Kuu ya Morogoro,” alisema Cheyo.
Kwa
wateja wa malipo ya fedha taslimu, mara baada ya mtu kulipa malipo ya
awali katika akaunti ya Bayport iliyopo Bank of Africa (BOA) na
kukabidhi nakala ya malipo na fomu za maombi kwa wakala au ofisi ya
Bayport, mteja atatengewa eneo kutokana na maombi yake na kuombwa
kumalizia kiasi kilichosalia, huku hati ya umiliki wa kiwanja akiipata
ndani ya siku 90 baada ya kumaliza malipo yake, na wanaotaka kupata
viwanja kwa njia ya mkopo kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni
binafsi na wajasiriamali, wakipata hati zao baada ya kumaliza mkopo wao.