AMANDA APIGWA ‘STOP’ NA BASATA!
S top! Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limemzuia Mwigizaji Tamrina Poshi ‘Amanda’ kufanya shoo aliyokuwa ameiandaa kufuatia kudaiwa ku...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/06/amanda-apigwa-stop-na-basata.html
Stop! Baraza la
Sanaa la Taifa (Basata) limemzuia Mwigizaji Tamrina Poshi ‘Amanda’
kufanya shoo aliyokuwa ameiandaa kufuatia kudaiwa kuwa kinyume na
maadili na makundi husika yalishapigwa marufuku.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Amanda alifunguka kuwa shoo hiyo ilikuwa ifanyike wikiendi iliyopita kwenye Ukumbi wa Mzalendo, Kijitonyama jijini Dar lakini ilishindikana kutokana na kupokea barua kutoka Basata ya kusitisha onesho hilo lililokuwa likiyahusisha makundi mawili ya Kanga Moko na Baikoko ambayo ni maarufu kwa kucheza nusu utupu.