TAA yashauriwa kuimarisha kiushindani Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere JNIA.
Mshauri Mkaazi wa ujenzi wa jengo la kufikia abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere akimwonyesha Naibu Katibu M...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/05/taa-yashauriwa-kuimarisha-kiushindani.html
Mshauri Mkaazi wa ujenzi wa jengo la kufikia abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere akimwonyesha Naibu Katibu Mtendaji- Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Bibi. Florance Mwanri (Kulia) maendeleo mradi huo.
Uongozi wa Mamlaka za Viwanja vya
Ndege Tanzania wameshauriwa kuwa makini katika ujenzi unaoendelea wa jengo la
kutua na kupaa ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyere (JNIA).
Ujenzi huo unaotarajiwa kuongeza
uwezo wa uwanja wa mara tatu zaidi umejikita katika sehemu za maegesho ya
magari, sehemu ya abiria kupumzika, sehemu za abiria kupandia na kushuka kwenye
ndege, ofisi za uhamiaji na huduma zingine muhimu.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo
Bw. Suleiman S. Suleiman amesema kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) hapo awali kilikuwa
na uwezo wa kuruhusu ndege sita tu kutua kwa saa lakini kwa sasa unaweza
kuruhusu ndege hadi 30. Tunatarajia kuongeza ndege zaidi na hivyo kuufanya
kiwanja hiki kuhimili 2500 tofauti na abira 700 wa awali pindi ujenzi huu
utakamilaka.
Kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 85, katika awamu ya kwanza
ambayo inategemewa kukamilika Juni mwaka 2016 na itakiwezesha JNIA kuhudumia
abiria milioni tatu na nusu kwa mwaka. Iwapo ujenzi wa awamu ya pili
utakamilika mwaka 2017 JNIA kitakuwa na uwezo wa kuhudumia jumla ya abiria
milioni sita kwa mwaka.
Alipokuwa akitembelea mradi huo,
Naibu Katibu Mtendaji- Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Bibi. Florance Mwanri,
aliuambia uongozi wa Mamlaka hiyo kuzingatia wazo la kuwa na huduma zote za
msingi katika kiwanja cha Julius Nyerere ili kuweza kushindana viwanja vya nchi
jirani na barani Afrika kwa ujumla.
“Ni vema kuwa kiwanja chetu cha
ndege kinapanuliwa ili kiweze kuhudumia watu wengi zaidi, lakini nimegundua
kuna vitu muhimu vimesahaulika katika usanifu wa upanuzi huu, kuna vitu kama
hoteli, jengo la hospitali, sehemu za kupata huduma za kibenki na pia namna
nzuri ya kuwapatia abiria watuao usafiri wa kwenda mjini na sehemu nyinginezo,
nadhani haya pia yazingatiwe, alisema Bibi. Mwanri.
Uwepo wa huduma hizi utawavutia
abiria kutumia kiwanja chetu kuliko vya majira zetu na pia kutakuza mapto ya
TAA na taifa kwa ujumla.
Ujenzi huu unaoendelea
umezingatia haja ya kuunganisha majengo yote matatu ili kurahisisha
uunganishaji wa ndege za ndani na za nje pia upokeaji wa mizigo.
Serikali kupitia Tume ya Mipango,
imeshaanza kuandaa Mpango wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 wenye dhima ya kukuza
uchumi wa kiviwanda hivyo basi Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege inapaswa kuwa chachu ya mpango huu kwa kusafirisha
watu na bidhaa zitakazozalishwa na viwanda hivyo”alisema Bibi. Mwanri.