KIBA AWASIHI MASHABIKI WAKE.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abdi Kiba, amesema mashabiki wake wakae tayari kupokea kibao chake kip...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/05/kiba-awasihi-mashabiki-wake.html
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abdi
Kiba, amesema mashabiki wake wakae tayari kupokea kibao chake kipya
kwani kitakuwa ni tishio.
Alisema juzi, kuwa alikuwa kimya tangu mwaka jana, sasa amevunja ukimya kwa kazi ambayo ataileta kwenu.
Kiba alisema anajua kwa sasa kuna
ushindani mwingi, hivyo anapaswa kuchukua muda kuandaa kazi nzuri na si
kukurupuka na kuitoa kitu kibaya.
“Kazi nzuri haihitaji haraka, inatakiwa
kuchukua muda ili kuweza kuiandaa na kuiachia kwa watanzania wakiwa
wanaielewa na si kufanya haraka ili kuingia kwenye ushindani,”alisema
Kiba alisema amekaa kwa muda mrefu kuandaa kazi hiyo, anaamini kwamba mashabiki wataikubali.