HUU NDIO UPENDO WA AUNT EZEKIEL KWA MTOTO WAKE.
Mwigizaji wa filamu nchini, Aunt Ezekiel amesema mtoto wake, anamfananisha na mboni ya jicho lake. Aunt amesema amefurahi ku...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/05/huu-ndio-upendo-wa-aunt-ezekiel-kwa.html
Mwigizaji wa filamu nchini, Aunt Ezekiel amesema mtoto wake, anamfananisha na mboni ya jicho lake.
Aunt amesema amefurahi kujifungua salama
na jukumu lililoko mbele yake ni kumlea na kumtunza mwanae ili aweze
kukua katika mazingira bora.
Akizungumza kutoka jijini Dar es Salaam,
Aunt alisema nguvu zake zote atazielekezea kwa mtoto wake kwasasa ili
kufanya jitihada kuhakikisha mtoto wake anaishi katika mazingira mazuri.
“Nina furaha sana na mimi kuitwa mama
kwani ndio ilikuwa ndoto yangu, nimeitimiza cha msingi sasa ni kumlea
mwanangu katika maadili mazuri tena ya kiafrika sijui niielezeje furaha
yangu asante mungu,”alisema
Aunt alijifungua mtoto wa kike alhamisi iliyopita na amempa jina la Cookie.
Baba yake ni Moses Iyobo, mnenguaji wa Diamond.