UEFA KUMUANGUSHIA RUNGU PEP GUARDIOLA
Shirikisho la soka Ulaya UEFA limemfungulia mashtaka kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola kwa kosa la kuvaa fulani a...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/04/uefa-kumuangushia-rungu-pep-guardiola.html
Shirikisho
la soka Ulaya UEFA limemfungulia mashtaka kocha wa Bayern Munich Pep
Guardiola kwa kosa la kuvaa fulani ambayo ilikuwa na ujumbe ambao
ulionekana kuvunja sheria za shirikisho hilo.
Kocha
huyo katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mechi ya marudiano
dhidi ya Porto alivaa fulana iliyoandika "Justiciaparatopo" ambao ni
ujumbe unachochea kampeni ya kutaka uchunguzi wa kifo cha mwandishi wa
habari Jorge Lopez ufanyike.
Mwandishi
huyo wa habari za michezo wa Argentina alifariki julai mwaka jana
katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil baada ya teksi aliyokuwa
amepanda kugongwa na gari ambalo lilikuwa limeibwa wakati likikimbizwa
na polisi.
Shirikisho
hilo limesema kuwa litatoa adhabu hiyo kwa kocha huyo baada ya kukiuka
sheria za kimichezo. "Mimi niliamka asubuhi, familia ilinipa fulana
,hivyo nikavaa,sioni kama kuna kosa lolote " alisema Guardiola.
Kikosi
cha kocha huyo kimefuzu hatua ya nusu fainali katika michuano ya klabu
bingwa Ulaya baada ya kuitoa FC Porto kwa jumla ya goli 7 kwa 4 katika
hatua ya robo fainali siku ya jumanne ya wiki hii.
