Picha: Bilionea Namba Moja Africa Dangote Akagua Ufukwe Atakao Jenga Bandari yake ya Kisasa Mtwara
https://samchardtz.blogspot.com/2015/04/picha-bilionea-namba-moja-africa.html
Biionea
Alhaji Aliko Dangote amekabidhiwa hekari 2,500, katika halmashauri ya
Wilaya ya Mtwara ili ajenge bandari itakayotumika kusafirisha saruji
kutoka kiwandani hapo kwenda maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.
Mfanyabiashara
maarufu Afrika, ambaye ni Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda
vya Dangote Group of Industries, Alhaji Aliko Dabgote akinyoosha mkono
kuangalia eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi katika Kijiji cha Mgao, Kata
ya Maumbu, Tarafa ya Mayanga, Mtwara Vijijini, ambapo atajenga bandari
yake ya kisasa kwa ajili kusafirisha saruji itakayozalishwa kwenye
kiwanda chake kikubwa kinachojengwa katika Kijiji cha Msijute.
Alhaji Dangote akishuka kwenye ndege na kulakiwa na Mwakilishi Mkazi wake hapa nchini, Esther Baruti
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Mgao, Shaa (kushoto) akimuonesha Dangote eneo la uwanja
aliopewa na wanakijiji kwa ajili ya ujenzi wa mkazi yake. Kijiji nacho
kitanufaika na Dangote ambaye atawajengea shule, hospitali pamoja na
miradi mingine ya maendeleo
Msafara wa Dangote ukitumia magari kutembelea kiwanda cha saruji kinachojengwa