Kajala: Nina Kibarua Kumchunga Paula
Staa mrembo wa Bongo Movies, Kajala Masanja ‘Kay’ amefunguka kuwa kwa umri aliofikia mwanaye, Paula...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/04/kajala-nina-kibarua-kumchunga-paula.html
Staa mrembo wa Bongo Movies, Kajala Masanja ‘Kay’ amefunguka kuwa kwa umri aliofikia mwanaye, Paula Paul wa miaka 14 ana kibarua kigumu cha kuhakikisha anakuwa salama hasa kwenye suala la wanaume.
Akiongea na gazeti la Ijumaa Wikienda hivi karibuni, Kajala alisema kuwa kwa umri huo, Paula ambaye alizaa na Prodyuza wa Bongo Records, Paul Matthysse ‘P Funky’ anahitaji uangalizi wa nguvu na kumsimamia kwa kila jamabo ili kuwakwepa ‘mijitu mikware’ ambao wanaweza kumrubuni.
“Dunia ya sasa watu siyo wema kihivyo lakini naamini sitashindwa na Mungu anisimamie,” alisema Kajala.