AL SHABAAB WACHINJA WANAFUNZI WANAOWASHIKILIA KATIKA JENGO LA CHUO KIKUU CHA GARISSA KENYA
Baadhi ya wanafunzi waliouawa au kujeruhiwa darasani Katika style kama ile ya shambulizi la Westgate Mall, wanamgambo wa al-Shabaab w...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/04/al-shabaab-wachinja-wanafunzi.html
Mkuu wa jeshi la polisi
Kenya, Inspector General Joseph Boinnet amesema kuwa magaidi hao
walivamia geti kuu la chuo hicho na kuwarushia risasi walinzi alfajiri
saa 5.30, wakati wanafunzi wa Kiislam wakienda kwenye swala ya asubuhi.
Polisi waliokuwepo
chuoni hapo walikimbilia katika eneo la tukio na kuanza kurushiana
risasi na magaidi hao, ambao walifanikiwa kuingia kwenye mabweni ya
wanafunzi.
Polisi wa ziada na wanajeshi waliitwa kuja kusaidia na mirindimo ya risasi ilisikika kati ya wavamizi hao, polisi na wanajeshi.
Wanafunzi waliokuwa wakipiga simu kutoka ndani ya mabweni wamesema kuwa kuna majeruhi wengi sana.
Wanafunzi waliofanikiwa
kutoroka wamesema kuwa idadi ya wavamizi hao ni angalau watano na bado
kuna wanafunzi na maprofesa wengi wanashikiliwa mateka.
Taarifa za hivi punde zinaarifu kuwa magaidi hao wameanza kuwachinja baadhi ya mateka waliowashikilia.
Mateka mmoja
(mwanafunzi) mwenye asili ya Somalia aliyeachiwa huru na magaidi hao
ameviambia vyombo vya habari vya Kenya kuwa wanafunzi kadhaa
wamekwishauawa na miili yao imetapakaa ndani ya vyumba na madarasa huku
zoezi la Uchinjaji wa mateka wengine walio hai likianza.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi hilo.
Kenyatta amewataka wakenya kuwa watulivu wakati huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao.
Wanajeshi wa jeshi la Kenya katika geti la chuo hicho |
Baadhi ya miili ya marehemu waliouawa katika shambulio la al-Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa |
Helicopter ya jeshi ikitua na maiti na baadhi ya majeruhi katika kambi ya jeshi la Langata |
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Excel, iliopo karibu na chuo kikuu cha Garissa wakiondolewa kutoka shuleni kuhakikisha usalama wao |