Flatnews

Uingereza kupambana na Ugaidi nchini Kenya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. Nchi ya Uingereza imesema itasaidiana na Kenya katika kukabiliana na ma...


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Nchi ya Uingereza imesema itasaidiana na Kenya katika kukabiliana na makundi ya kigaidi ili kuboresha amani kama njia bora ya kukuza uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili.

Kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond amesema hayo baada ya Kenya na Uingereza kutia saini mkataba wa maelewano baina ya mashirika ya biashara na viwanda vya nchi hizo mbili.
Wafanyabiashara wa Uingereza na Kenya wamepongeza kutiwa saini kwa mkataba wa kibiashara kati ya nchi zao. Hamond amesema ukosefu wa usalama unatishia kuvuruga biashara kati ya nchi hizo mbili.
Hafla hiyo iliongozwa na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Phillip Hammond na mwenzake wa Kenya Amina Mohamed.
Kuwasili kwa Hamond nchini Kenya kuliashiria kuwa Uingereza imeanza kuukubali utawala wa Rais Kenyatta.
Naye  waziri wa mambo ya nje wa Kenya balozi Amina Mohamed alisema kuwa hatua ya Uingereza kuwapiga marufuku raia wao kuzuru Kenya kutokana na msururu wa mashambulizi ya kigaidi umeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii.

Related

NEWS 4683321925571173755

Post a Comment

emo-but-icon

item