PHOTOS; RIHANNA AKIWA UFARANSA AKILA BATA KWA MRIJA
Yanawahu? Fuata nyuki upate manundu Msanii nyota wa Marekani, Rihanna ameendelea kuwa ‘bize’ katika ziara zake za kula bata k...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/03/photos-rihanna-akiwa-ufaransa-akila.html
Yanawahu? Fuata nyuki upate manundu
Msanii nyota wa Marekani,
Rihanna ameendelea kuwa ‘bize’ katika ziara zake za kula bata katika
maeneo mbalimbali yanayosifika kwa kuponda maraha duniani.
Akiwa na rundo la wapambe
wake, Rihanna ameshajirusha sana katika maeneo ya kujidai ya jiji la New
York, akaenda zake Barbados, akatua nchini Italia na sasa yuko katika
fukwe za kusini mwa Ufaransa, akiendelea kujiachia kupita kiasi na
wapambe wake ndani ya boti ya kifahari.
Tazama baadhi ya mapicha
yake aliyopigwa jana wakati yeye na wenzake wakila, kukata kilaji,
kuvuta sigara, kuimba, kukata mauno sanaaaa na kasha kujimwaga baharini
na vijaketi maalum vya kuogelea na pia kuendesha ‘pikipiki’ za baharini.
Mchumu mchumu, mchumu tena....mmwaaa!
Chezea Rihanna weye... nani anamuweza kwa mauno?
We unageuka kwangu kuna nini? Si uendelee na mambo yako!
Hapa Rihanna keshaanza kuwa bwaksi....bila shaka anaimba: "... nataka paja miee.. hakinitoshi kipapatio!
Hapa mrembo kakalia nini? Kigoda cha Rihanna!
Usiangalie utapofuka!
Mitungiii, blantiii, mikasii...ooh yeah!
Wewweeeeeehhh....!
Twende nikupe lifti