MEYA MANISPAA KINONDONI ATEMBELEA MABONDENI, AWATAKA WATU KUHAMA KUOKOA MAISHA YAO
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kushoto) akimsikiliza Naibu Meya, Songoro Mnyonge wakati akimpa maelezo kuh...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/03/meya-manispaa-kinondoni-atembelea.html
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (wa pili kushoto) akimsikiliza
Naibu Meya, Songoro Mnyonge wakati akimpa maelezo kuhusu mazingira ya
Mto Kiboko uliopo katika Kata ya Tandale wakati wa ziara yake katika
Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana.
Mkazi
wa Mtaa wa Bahi, Jomo Macha akimueleza Meya wa Manispaa ya Kinondoni,
Yusuph Mwenda athari za mafuriko katika Mtaa huo, Kata ya Makumbusho
wakati wa ziara ya Meya huyo jana. Wengine ni Watendaji wa Manispaa hiyo
na wakazi wa eneo hilo.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akitoa maelekezo kwa watendaji
wa Manispaa hiyo kuhusu kutafuta ufumbuzi wa chemba ya majitaka
iliyofurika katika Mtaa wa Balozi Msolomi wakati wa ziara yake. Kulia
kwake ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge na watendaji wa Manispaa hiyo.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (mbele) akikagua mto Ng'ombe
uliopo eneo la Mwananyamala Kisiwani, wakati wa ziara hiyo Nyuma yake ni
Naibu Meya,Songoro Mnyonge.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) akijadiliana jambo na
Naibu Meya, Songoro Mnyonge wakati wa ziara aliyoifanya katika Mtaa wa
Kimamba, Kata ya Makurumla kukagua athari za mafuriko na changamoto zake
jana. Katikati ni Diwani wa Kata hiyo, Rajab Hassan.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kulia) akikagua athari za
mafuriko katika moja ya nyumba za Mtaa wa Kimamba, Kata ya Makurumla
alipofanya ziara yake katika Manispaa hiyo, Dar es Salaam jana. Kushoto
ni Diwani wa Kata hiyo, Rajab Hassan.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Kimamba, Kata ya Makurumla, Mohamed shukuru
akisisitiza jambo kwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
kuhusu mikakati wanayoifanya kuepuka mafuriko wakati wa ziara ya Meya
huyo aliyoifanya katika Mtaa huo jana. Kushoto ni Naibu Meya, Songoro
Mnyonge na Diwani wa Kata hiyo, Rajab Hassan.
Msafara wa Meya wa Kinondoni ukijiandaa kuondoka eneo la Mto Ng'ombe baada ya kukagua mto huo, eneo la Mwananyamala Kisiwani.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MEYA
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda amewataka wakazi kwenye mikondo
ya maji wahame haraka kwa usalama wa maisha yao na si kusubiri
waondolewe kwa nguvu.
Mwenda
alisema tayari baadhi ya wakazi wa maeneo hayo walishalipwa fidia na
kutafutiwa maeneo mengine na Serikali lakini wamerejea na kuendelea na
maisha yao jambo ambalo alisema sasa Manispaa yake haitasita kuwaondoa
kwa nguvu.
Akizungumza
wakati wa ziara yake aliyoifanya katika maeneo ya mabondeni na mikondo
ya maji katika Manispaa hiyo Dar es Salaam jana Meya huyo alisema
anashangaa kuona watu wanajenga makazi katikati ya mkondo wa maji na
kusababisha maji hayo kukosa uelekeo na kuingia kwenye makazi yaw engine
hususan kipindi hiki cha mvua ilhali tayari walishaondolewa.
“Mfano
watu wa Kinondoni Hananasif na Suna tayari walishapewa fidia na kupewa
viwanja, lakini wengi wao wameshauza viwanja hivyo na kurudi tena maeneo
hayo. Hii inashangaza sana. Tunafanya hivi kwa faida ya maisha yao
hatutaki kuona watu wanakufa yanapotokea mafuriko.” Alisema Meya Mwenda.
Mwenda
alifanya ziara hiyo katika Kata za Makurumla, Tandale, Makumbusho na
Mwananyamala na kushuhudia baadhi ya wakazi wakiwa wamejenga nyumba zao
katikati ya mikondo ya maji na kusababisha maji kukosa uelekeo na
kuingia katika makazi ya watu ikiwemo Mtaa wa Kimamba eneo la Daraja la
Mwinyi.
Katika
hatua nyingine Meya huyo alimwagiza Mhandisi Mkuu wa Manispaa hiyo
kuwasiliana na Wahandisi wa kampuni ya ujenzi ya Strabag kupata ufumbuzi
wa tatizo la mifumo ya majitaka inayopita kwenye barabara hiyo
kutafuta njia ya kupeleka maji hayo ili kuzuia yasiingie katika makazi
ya watu hususan katika kipindi hiki cha mvua.
Hata
hivyo Meya huyo amesifu jitihada za wataalamu wa Manispaa hiyo kwa
kushirikiana na watendaji za kuhakikisha wanasafisha njia za maji
ikiwemo mitaro ma mito mbalimbali akitolea mfano Mto Ng’ombe uliopo
Mwananyamala Kisiwani ambao awali ulikuwa ukifurika maji na kusababisha
mafuriko maeneo mbalimbali ikiwemo Tandale kwa Mtogole kutokana na kujaa
taka ukilinganisha na sasa.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda alifanya ziara yake katika maneo
mbalimbali ya mabondeni na kwenye mikondo ya maji yaliyopo kwenye
Manispaa hiyo Dar es Salaam jana ili kuona athari za mafuriko
zilizojitokeza kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha jijini kwa lengo la
kutafuta ufumbuzi wa kuepukana na mafuriko hayo.