Benki ya Posta yawapa msaada waathirika wa mvua ya mawe Kahama
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya
https://samchardtz.blogspot.com/2015/03/benki-ya-posta-yawapa-msaada-waathirika.html
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi (kulia)
akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa
Benson Mpesya (kushoto) msaada wa tani saba na nusu za saruji kwa
waathirika wa mafuriko yaliyotokana na mvua yam awe yaliyotokea kijiji
cha Mwakata Wilaya ya Kahama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Benson Mpesya
(kulia) akitoa shukrani kwa Benki ya Posta mara baada ya kupokea msaada
wa tani saba na nusu za mifuko ya saruji zilizotolewa na benki hiyo.
Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi akizungumza
na wajumbe wa kamati ya maafa kabla ya kukabidhi msaada uliotolewa na
benki hiyo.
Na Mwandishi Wetu
BENKI
ya Posta tawi la Shinyanga imetoa msaada wa mifuko ya saruji tani saba
na nusu yenye thamani ya sh. milioni 3 kwa ajili ya waathirika wa mvua
ya mawe katika Kijiji cha Mwakata wilaya ya Kahama.
Msaada
huo umekabidhiwa jana na Meneja wa Tawi la Benki ya Posta, Shinyanga
Lawrence Munisi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa na Mkuu wa Wilaya ya
Kahama, Benson Mpesya.
Akikabidhi msaada huo Meneja wa Tawi la Benki ya Posta Shinyanga,
Lawrence Munisi alisema Benki ya Posta imeguswa na tukio zima la maafa
ya mafuriko na mvua ya mawe iliyoleta madhara kwa wananchi hivyo imeamua
kuchangia msaada wa mifuko ya saruji isaidie kwa wananchi walioathirika
na janga hilo.
“Kwa
niaba ya Benki ya Posta, tunatoa pole kwa wale wote waliokumbwa na maafa
haya ya mafuriko, na kwa msaada huu wa mifuko ya saruji tunaamini
inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa sana waathirika wote,” alisema Munisi
akikabidhi msaada huo.
Aidha
kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya
Maafa, Mpesya alitoa shukrani za dhati kwa niaba ya waathirika wote na
kuziomba taasisi nyingine na hata watu wenye uwezo kuiga mfano wa Benki
ya Posta.
“Kwa
kweli tunashukuru sana kwa msaada huu mliotoa Benki ya Posta, na
tunaamini msaada huu utasaidia sana katika kurudisha mazingira mazuri
kwa wale wote waliopatwa na maafa haya...Tunaomba pia taasisi nyingine
ziunge mkono, maana hili janga ni la Taifa na takribani watu wengi sana
wamepoteza malazi na mahitaji yao mengine muhimu," alisema Mpesya.
Mvua
kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha hivi karibuni
katika Kijiji cha Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga ilisababisha
maafa ambako watu kadhaa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa. Nyumba
kadhaa zilianguka na nyingine kuezuliwa paa kutokana na upepo mkali
ambapo baadhi ya familia zimekosa makazi.