Flatnews

Waziri Nyalandu Afungukia Mimba ya Aunt Ezekiel

Hatimaye Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Samwel Nyalandu na mkewe Faraja Kotta hivi majuzi wamejibu t...


Waziri Nyalandu Afungukia Mimba ya Aunt Ezekiel
Hatimaye Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Samwel Nyalandu na mkewe Faraja Kotta hivi majuzi wamejibu tetesi kuwa mheshimiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson.

Awali tetesi hizo zilieleza kwamba Nyalandu na Aunt walikutana nchini Marekani kwenye hafla ya ubalozi wa Tanzania nchini humo.
Akizungumza na kituo cha Redio, Nyalandu  asisitiza kuwa hili ni jambo ambalo alipenda mno kulitolea ufafanuzi kwa kuwa lilipoandikwa watu wake wa karibu walimuuliza pia kutaka kufahamu kama kuna ukweli wowote.
“Unajua mpaka nikaanza kucheka,” alisema Nyalandu.
“Unajua watu wana midomo, watu wanaweza wakachonga lakini michongo mingine inaweza ikawa haina dili kabisa.
“Hata anayechonga pia anajua anasababisha zogo ambalo anataka lizae matunda na wanajaribu kuliendeleza.
“Nilifika kama mgeni rasmi kwenye tukio ukiwa mwaliko wa ubalozi na tukio lile lilichukua saa moja na huyo dada anayeitwa Aunt Ezekiel katika maisha yangu nimemuona siku moja, ndiyo hiyohiyo siku nimemuona, nilikuwa sijawahi kumuona tangu nizaliwe.
“Tumekutana naye akiwa mwalikwa pamoja na maDJ wengine wa Bongo Fleva katika tukio lenye watu wengi ambao ni Watanzania waishio Marekani.
“Nikiwa mgeni rasmi nikatoa vyeti, nikatoa hotuba wakanisindikiza nikaondoka. Kwa hiyo kwanza katika hali hiyo ya kuwa Amerika (Marekani) atakuwa aliniona kwa saa moja kwenye ule mkutano.
 “Lakini pia nilikuwa sijawahi kumuona katika maisha yangu na sijawahi kumuona tena, yaani ni mtu ambaye sifahamiani naye,” alisema Nyalandu pembeni akiwa na mkewe.

Related

PHOTOS 1098817776745880815

Post a Comment

emo-but-icon

item