Lucy Komba Anyoa Rasta Kisa Ndoa
Muigizaji wa filamu za Kibongo, Lucy Komba ambaye hivi karibuni alifunga ndoa na Janus Stanley, raia wa Den...
https://samchardtz.blogspot.com/2015/02/lucy-komba-anyoa-rasta-kisa-ndoa.html
Muigizaji wa filamu za Kibongo, Lucy Komba ambaye hivi karibuni alifunga ndoa na Janus Stanley, raia wa Denmark, amesema kuwa ameamua kunyoa rasta zake alizozifuga kwa muda mrefu kwa kile alichodai matakwa ya ndoa.
Akizungumza na mwandishi GPL, Lucy alisema kuwa ameamua kunyoa nywele zake hizo kwa kuwa anaona ni mke wa mtu anatakiwa kubadilika na kuwa tofauti kidogo na alivyokuwa huko nyuma.
“Unajua lazima kuwe na tofauti kidogo, zamani na sasa, hivyo nimeamua kunyoa kuleta utofauti,” alisema Lucy.